Mashambulizi mawili ya Mpeketoni yalisababisha vifo vya watu 60 na kuacha vuta n’kuvute nchini Kenya baada ya Al Shabab kudai kuhusika moja kwa moja na huku serikali ya rais Kenyatta ikipinga na kuwa wanyoshea kidole wanasiasa wa upinzani.
Al Shabab walidai wamefanya tukio hilo kulipiza kisasi kufuatia maamuzi ya Kenya kupeleka wanajeshi wake nchini Somalia kulisaka kundi hilo.
Zaidi ya wananchi 4,000 wa Kenya kupitia Twitter wameanzisha kampeni yenye hashtag#BringBackOurKDFSoldiers ili kushinikiza serikali yao kuwarudisha nyumbani wanajeshi wao kutoka Somalia.
Wanajeshi wa Kenya wako nchini Somalia tangu mwaka 2011.
Raila Odinga alisikika jana akitoa wito kwa rais Uhuru Kenyatta kuitisha kikao cha pamoja na wapinzani ili kujadili kuhusu maswala ya usalama wa nchi hiyo ikiwa ni pamoja na uamuzi wa kuendelea kulitumia jeshi lao nchini Somalia.
#BringBackOurKDFSoldiers inatoka kwenye hashtag maarufu zaidi duniani kwa kipindi hiki iliiyoanzia Nigeria kuwataka wanajeshi kuwarudisha wasichana wa Nigeria walitekwa na kundi la Boko Haram #BringBackOurGirls.

No comments: