» » MESUT OZIL AANZA RASMI MAZOEZI ARSENAL


ozil_fb481.jpg
MESUT OZIL AANZA RASMI MAZOEZI ARSENAL HUKU FAMILIA YAKE IKITISHIA KUISHTAKI REAL MADRID
Familia ya mchezaji Mesut Ozil imetishia kumshataki raisi wa Real Madrid Florentino Perez juu ya madai kwamba mahusiano yake na mrembo wa kivenezuela yalimfanya ashuke kiwango alipokuwa Santiago Bernabeu.(P.T)
Baba yake Ozil, Mustafa alimshambulia vikali Perez, huku mwanae akiwa anatambulishwa rasmi kwenye klabu yake ya Arsenal na kuanza mazoezi, Mr. Mustafa Ozil alisema kwamba hatua za kuanza kumshtaki zimeanza.
Mzee huyo ameonekana kukasirishwa vibaya kufuatia taarifa zilizochapishwa na gazeti la kihispania Marca kwamba Perez amesema kiwango cha Ozil akiwa na Real Madrid kilishuka kufuatia kuhangaika kwake na mpenzi wake ambaye ni mrembo wa zamani wa Venezuela, Aida Yespica.
Ozil Snr pia alikasirishwa na mawazo kwamba ubinafsi wake wa kutaka fedha nyingi zaidi ndio uliochangia mjerumani huyo kujiunga na klabu ya Arsenal akitokea Madrid.
'Ni wazi Perez sio mwanadamu mwenye heshima, anaweza kuwa na fedha nyingi lakini hilo halimfanyi kuwa mtu mwenye heshima na adabu.
'Anajaribu kufanya kwamba Mesut hakuwa mweledi kutoka na staili ya maisha yake akiwa Madrid na mimi baba yake nina uroho wa fedha tu. Haya yote ni ya uongo, na ndio maana nafikiria kumshtaki.
'Tutaangalia kila kitu, mawakili wameanza kuangalia kama kesi itakuwa na nguvu au la kabla ya kuangalia mbele, na baada ya hapo tutaamua hatua za kisheria za kuchukua.
'Anataka kumgeuza Mesut mbuzi wa kafara na kuonyesha kwamba ana mzazi mroho wa fedha, wakati hay mambo yapo mbali na ukweli. Tupo tayari kujitetea, kwa sababu ninachokitaka kwa mwanangu ni kufanikiwa. Hilo ndilo limekuwa jukumu langu siku zote.'
Chanzo:shaffihdauda 

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply