» » » Mambo usiyoyajua kuhusu Zamaradi Mketema wa Take One ya Clouds Tv

Kumekuwa na rumors nyingi zikienea hapa town kila mtu akisema lakwake juu ya uchanganyiko wa utaifa wa Zamaradi kutokana tu na muonekano wake ,huku wengi wakiotea kuwa ana asili ya usomali,ila ukweli ni kwamba ,Baba yake mzazi Zamaradi ni Mmanyema kutoka Kigoma, wakati mama yake mzazi ndiye mwenye asili ya kinyarwanda,kwahiyo Zamaradi ni Mmnanyema kabisa kutoka huko Kigoma.Alishawahi kushiriki U-miss akiwa bado mwanafunzi wa chuo cha St.Augustine ya Mwanza,ingawa haikuwa kazi rahisi kwake kuweza kukubali mara moja,kuingia katika mashindano hayo,ila kutokana na ushauri wa rafiki zake wakaribu ,akiwemo mama yake mzazi, kumshawishi ,ndipo alipoamua kuingia katika mashindano hayo.
Mbali na kuchelewa kuingia kambini na kuanza mazoezi na kupitia harakati nyingi za mawazo za kukubali mwisho wa siku alifanikiwa kushika nafasi ya kwanza na kuchukua taji la Miss Mwanza mwaka 2007.


Kutokana na imani kali ya kidini aliokuwa nayo baba yake ,ile baada tu ya kushinda U-miss,alipokea simu kali sana kutoka kwa baba yake mzazi na kugombezwa sana,cause hakuwa na taarifa juu ya ushiriki wa mwanaye katika maswala ya urembo ,na kutokana na kile kwamba baba yake wakati wa uhai wake alikuwa ni mtu wa dini sana.
Ingawa akiwa bado mdogo, alitamani sana aweze kukua mapema nakuanza maisha yake mwenyewe,baada ya mama yake mzazi kufariki dunia, Zamaradi Mketema akiwa bado ni msichana tu,aliachiwa mzigo mkubwa wa kumlea mdogo wake wa pekee aitwaye Ummy,yeye akiwa kama ndiye dada ,mama na baba wa pekee nyumbani hapo,hadi hivi sasa kuweza kufika mahali anajitegemea mwenyewe na cha zaidi kujaliwa mtoto wake wa kiume aliyempa jina la Junior.Hekaheka za mitaani kwenye kipindi cha Leo tena cha cloudsFm,ndiyo iliyoweza kumpa mawazo ya ubunifu ya kufanya movie yake ya Kigodoro,katika kukaa na kusikiliza matukio mengi yanayotokea sana mtaani kupitia section ya hekaheka za mitaani,aliweza kupata wazo lililoweza kumuweka chini na kutunga story ambayo mwisho wa siku ,ndio imeweza kuzaa movie ya Kigodoro,movie iliyogharimu shilingi milioni 18 hadi kuingia sokoni.Kigodoro moja kati ya movie ambayo ,imeleta mapinduzi makubwa katika tasnia nzima ya Bongo Movie,kutokana na ubora katika uigizaji,uwezo wa hali ya juu wa wasanii waliocheza ndani ya movie hiyo na ubora wa utengenezaji mzima wa hiyo movie, ndicho kinachofanya Kigodoro iwe gumzo hapa tow

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply