Fikiria unapokosa usingizi kwa usiku mmoja tu na jinsi utakavyojisikia vibaya siku inayofuata? Je! Vipi kama ukikosa kabisa usingizi kwa siku 60 mfululizo? Unaweza kuchanganyikiwa bila shaka. Lakini hali hiyo ilimkuta hayati Michael Jackson ambaye leo anatimiza miaka minne tangu afariki dunia.
Dr Charles Czeisler, mtaalam wa usingizi, aliwaambia wazee wa Mahakama wakati wa kesi inayoendelea juu ya kifo chake cha utata kuwa supastaa huyo anaweza kuwa mtu wa kwanza kuwa na rekodi ya kumaliza siku 60 bila kupata usingizi.
Aliyekuwa daktari wake, Conrad Murray anadaiwa kumpa Jackson kwa miezi miwili dawa hatari ziitwazo Propofol ili zimpatie usingizi usingizi. Dawa hizo zinadaiwa kumfanya mtu alale bila kujitambua na sio kumfanya apate usingizi wa kawaida.
Czeisler alieleza kuwa dalili za kuwa Michael hakuwa analala kama vile kusahau maneno kwenye nyimbo zake ama kuwa na uwezo wa kucheza zilikuwa ni kawaida kwa mtu anayesumbuliwa na tatizo la kukosa kabisa usingizi kwa muda mrefu.
Aliendelea kudai kuwa kama muimbaji huyo asingepoteza maisha kwa kuzidisha dawa angeweza kufa kwa kukosa usingizi.Familia ya Michael inaishitaki kampuni AEG concerts iliyokuwa imemwajiri Murray na kutaka ilipwe dola bilioni 26.
Mwezi huu kesi hiyo ilionekana vituko baada ya CEO wa AEG, Randy Philipps alitoa ushahidi kuwa amekuwa akizungumza na ‘mzimu’ wa Michael. Alidai kuwa rafiki yake MJ ambaye ni mke wa Lionel Ritchie, Brenda, amekuwa akiwasiliana na mzimu huo moja kwa moja ama kwa simu. Brenda alidai kuwa Michael amemwambia kuwa Dr Murray hana kosa kwakuwa alijiua kwa bahati mbaya.
No comments: