Lionel Messi akidhibitiwa (HM)
KOCHA wa Bayern Munich, Pep Guardiola ameifunga timu yake ya zamani, Barcelona mabao 2-0 katika mchezo wa kirafiki mjini Munich jana.
Philipp Lahm alifunga bao la kwanza dakika ya 14 na timu zikaenda kupumzika matokeo ya 1-0, kabla ya Bayern kupata bao la pili dakika ya 87 lililofungwa Mario Mandzukic.
Kikosi cha Bayern Munich kilikuwa: Neuer/Starke dk46, Rafinha, Dante/Van Buyten dk59, Boateng, Alaba, Thiago, Lahm/Gustavo dk59, Kroos, Ribery, Robben/Shaqiri dk46 na Muller/Mandzukic dk46.
Barcelona: Pinto/Oier dk46, Montoya/Kiko dk46, Bartra/Gomez dk46, Mascherano/Planas dk46, Adriano/Patric dk46, Song/Espinosa dk46, Sergi Roberto/Ilie dk46, Dos Santos/Quintilla dk46, Tello/Joan Roman dk46, Messi/Dongou dk46 na Alexis/Dani Nieto dk46.
Chanzo: sportsmail
No comments: