INAONEKANA Arsenal imepoteza nafasi ya kumsajili mshambuliaji wa kiargentina Gonzalo Higuain ambaye imemuwania kwa muda mrefu baada ya mshambuliaji kukaribia kujiunga na klabu ya Napoli ya Italia. (HM)
Kwa mujibu wa mtandao wa Sky News ni kwamba hivi sasa nchini Italia mshambuliaji Gonzalo Higuain na kipa wa Liverpool Pepe Reina ambaye nae alihusishwa na Arsenal huko nyuma wapo kwenye vipimo vya afya vya kujiunga na klabu ya Napoli.

Real Madrid na Napoli zimekubalina ada ya uhamisho wa Higuain kuwa kiasi cha £32million na kukubaliana na mchezaji mwenyewe mkataba wa miaka mitano kwa mshahara wa paundi 140,000 kwa wiki.
Chanzo: shaffihdauda
No comments: