Kama asingefanyiwa upasuaji wa hips mwaka huu kiasi cha kumfanya asitishe ziara yake, Lady Gaga angeingiza fedha nyingi zaidi. Lakini pamoja na hivyo, Queen Monster huyo ameingiza benki dola milioni 80 mwaka jana pekee na kumfanya aongoze orodha hiyo.
Kabla ya kuisitisha, ziara hiyo ilikuwa imeshaingiza dola milioni 168 hadi January mwaka huu. Kama angeweza kuimaliza angeingiza dola milioni 200.
Justin Bieber – Dola milioni 58
Justin Bieber – Dola milioni 58
Mwaka jana pekee, dogo huyu wa Canada alifanya ziara katika nchi kadhaa duniani, akajiongezea followers wengine milioni 20 kwenye Twitter na kuingiza dola milioni 58.
Taylor Swift – Dola milioni 55
October mwaka jana, Taylor aliachia albam yake, Red, na kuuza kopi milioni 1.2 kwenye wiki ya kwanza peke yake. Aliendelea kula mashavu ya matangazo kama ya Diet Coke, Sony na Covergirl.
Calvin Harris – Dola milioni 46
Calvin Harris aligundulika kwenye mtandao wa Myspace miaka minane iliyopita. Hadi leo, Harris amekuwa na jina kubwa kama Dj na producer. Mwezi February, alisainiwa kudj kwenye show zaidi ya 70 kwa kipindi cha miaka miwili jijini Las Vegas.
Pamoja na kwamba fedha zake nyingi zinatokana na kutumbuiza, pia ameingiza mtonyo wa nguvu kwa kuandika na kutayarisha hit single ya Rihanna, “We Found Love.” Harris ametumbuiza kwenye show zaidi ya 150 katika miezi 12 June 1, 2012.
Rihanna – Dola Milioni 43
Mrembo huyu wa Barbado anaendelea kupiga mkwanja wa nguvu kwa kutumbuiza kwenye show zaidi ya 40, na kuachia albam yake ya saba Unapologetic na biashara na deals zingine za matangazo.
Katy Perry –Dola milioni 39
Katy Perry –Dola milioni 39
Ukimtoa Michael Jackson, hakuna msanii mwingine zaidi ya Katy kuwahi kuwa na nyimbo tano za albam moja (Teenage Dream) zilizoshika nafasi ya kwanza kwenye chart duniani.
Ameendelea kuingiza mkwanja kwa kutumbuiza kwenye show binafsi, pafyumu yake Coty na mchongo wake na watengenezaji wa vitafunwa Popchips ambako pia ana hisa bila kusahau deals zingine.
Adele – Dola milioni 25
Muimbaji huyu wa Uingereza bado anaingiza fedha nyingi licha ya kwamba hajawahi kufanya tour kubwa ya dunia.
Jennifer Lawrence – Dola milioni 26
Hatujajua kwanini wamemweka nafasi hii wakati anamzidi dola milioni moja Adele lakini muigizaji huyo wa Hollywood’ mwaka jana aliingiza fedha nyingi kwa kuigiza filamu Silver Linings Playbook na The Hunger Games.
Kristen Stewart – Dola milioni 22
Pesa za Twilight zinaendelea kuingia. Ameigiza pia filamu zilizofanya vizuri kama Snow White na Huntsman.
Taylor Lautner – Dola milioni 22
Pesa za Twilight zinamhusu pia jamaa huyu. Hajafanikiwa sana kwenye miradi nje ya filamu za Twilight licha ya kuigiza kwenye filamu kama, Abduction na kwenye filamu ya Adam Sandler, Grown Ups 2.
No comments: