Pamoja na kwamba anategemea kusaini mkataba ‘mnono’ alhamisi wiki hii lakini weekend iliyopita aliambulia kuzomewa ‘boo’ na mashabiki wachache waliohudhuria show yake huko Kericho, Kenya.
Msala huo haukuishia hapo, inadaiwa kutokana na mahudhurio madogo ya mashabiki tofauti na matarajio ya muandaaji, Nice na Promota wake waliondoka Kericho kurudi Nairobi bila kulipana kwa kutimia gari binafsi ambayo nayo kwa mbaya mafuta yaliwaishia njiani na kuwasababisha wakwame njiani kwa muda mrefu kabla ya kupata msaada.
Sifa aliyonayo Mr Nice nchini humo kwa mujibu wa Daily Post ni kuwa yuko Kenya kutokana na historia ya sifa mbaya aliyonayo Tanzania iliyotokana na majivuno ‘arrogance’ na matumizi mabaya ya pesa aliyokuwa nayo kipindi jina lake lilipokuwa juu na kupelekea kuanguka kwake kimuziki.
SOURCE: DAILY POST
No comments: