Mchezaji mstaafu wa timu ya football ya Marekani, Baltimore Ravens, Ray Lewis wiki iliyopita alishindwa kuupanda Mlima Kilimanjaro kutokana kuumia mguu na kupata homa.
Lewis alikuja kuzitembelea nchini za Afrika Mashariki na juzi alikuwa Dar es Salaam ambapo pia alikutana na Rais Jakaya Kikwete aliyempa zawadi ya kofia ya timu ya Ravens.
Lewis alitumia muda wa saa nzima kuzungumza na Rais Kikwete ambaye alimwalika kuja tena Tanzania siku za usoni.
Mchezaji huyo yupo Afrika Mashariki kwenye mradi wa kusaidia upatikanaji wa maji safi na salama na ameongoza na mchezaji wa zamani wa Chicago Bears Pro Bowl, Tommie Harris na Doug Pitt, kaka yake na muigizaji Brad Pitt ambaye ni balozi mwema wa Tanzania.
Bila Lewis, kundi hilo lilifanikiwa kuupanda mlima huo mrefu zaidi barani Afrika wenye futi 19,340. Lewis na kundi lake walitoa msaada wa vifaa vya kusaidia watu wenye ulemavu wa kusikia na pia alitembelea kituo cha kulelea watoto yatima.
Ray akizungumza na mtoto
Ray na watoto
Ray akiwaonesha kitu watoto huko Moshi, Kilimanjaro
Pia mchezaji huyo alitumia muda wake na watoto hao ambao aliwaomba waandike mahitaji yao kwenye karatasi.
Kabla ya kuondoka, Lewis aliweka alama ya mkono kwenye ukuta wa darasa.
Baada ya kuona kuwa hawezi kupanda mlima Kilimanjaro kutokana na hali yake ya kiafya, Lewis alizungumza kwenye video kuhusu msaada wake kwa Afrika.
“Kitu kikubwa tulichonacho kwenye maisha ni fursa,” anasema Lewis. “Ni kwa kufanya kupitia fursa ndio kunaweza kuacha urithi usioisha. Timu hii tuliiweka kwenda kubadilisha maisha na maisha na kuwashika watu ambao hawatajua hata majina yetu lakini watakumbuka urithi wetu kutokana na kile tulichokifanya kuleta maji safi kwenye ardhi ya mama zetu kwa watu wasiojiweza na kuwapa fursa ya pili.”
Lewis, 38, aliyestaafu baada ya kushinda Super Bowl ya pili akiwa na Ravens, kwa sasa anafanya kazi na kituo cha ESPN kama mchambuzi wa football. Aliongozana na mashirika ya WorldServe International na TackleKili kwenye ziara hiyo.
No comments: