Hivi karibuni mama Blue Ivy Beyonce Knowles kutoka Marekani alionekana katika moja ya show zake za Mrs Carter World tour akiwa amevaa vazi la kanga lenye maneno ya kiswahili “Wawili Ninyi Yawahusu….” ambalo lilitengenezwa na mwanamitindo mtanzania Christine Mhando aishiye Uingereza.
Beyonce ameendelea kuvaa vitu vyenye asili ya Africa baada ya kupiga picha za jarida la Flaunt akiwa amevaa urembo wa Kiafrika ambao huvaliwa zaidi na watu wa kabila la kimasai hapa Tanzania.
Picha hizi za Beyonce akiwa amevaa kiafrika zilipigwa mwaka 2011 lakini haijulikani kwanini amekuja kuzitumia wakati huu.
No comments: