Mwakilishi wa Tanzania kwenye shindano la Big Brother Africa, Ammy Nando ameamua kusimulia mbele ya washiriki wengine masuala mazito na magumu aliyoyapitia kwenye familia yake.
Anasema baba yake aliwahi kulazwa katika hospitali nchini India na familia yao iliambiwa kuwa alifariki kwa ugonjwa wa kisukari lakini Nando hakushawishika na maelezo hayo.
“Baba yangu alikuwa na kampuni kubwa ya ujenzi iliyokuwa na caterpillars lakini vyote hivyo vilipotea,” alisema. Aligundua kuwa alitakiwa kwenda India mapema awezavyo kuliona kaburi la baba yake ili auridhishe moyo wake.
Kama hiyo haitoshi, mdogo wake kike naye alifariki lakini hakujua mahali alikozikwa na wala hajui pia mahala mama yake wa kambo alikozikwa. Anasema dada yake aliolewa na wala hawana ukaribu naye.
Kipindi walichowahi kuwasiliana ni pale tu dada yake alimpigia simu na mara nyingine pale alipowasiliana naye kupitia Facebook na akapotea tena.
Nando hajawahi kumuona mdogo wake wa kiume japo wamewahi kuwasiliana mara moja tu Facebook ambapo mdogo wake alimwambia kuwa anaendelea vizuri na ameanzisha kampuni yake.
Kwa mara nyingine tena Nando hakushawikisha na maelezo hayo sababu bibi yao alimwambia kuwa mdogo wake huyo ameendelea kutumia madawa ya kulevya na haaminiki kwakuwa aliwahi kuiba simu ya mfanyakazi wa ndani na kwenda kuiuza.
Mshiriki wa Kenya Annabel alimwambia Nando kuwa akitoka The Chase aende kumtafua dada yake na yeye kukubali kufanya hivyo.
Source: http://bigbrotherafrica.dstv.com
No comments: