Ni ukweli ulio wazi kuwa hit single ya ‘Sio Mimi’ au kwa jina lingine ‘Pombe Yangu’ ya Rais wa Manzese Madee kutoka Tip Top Connection ni miongoni mwa nyimbo za bongo fleva ambazo ni lazima uzisikie popote uendapo kama sio Radio zote, basi ni bar, club, kwenye bajaji na sehemu zote za burudani au kwenye TV, na Sasa anakuja na single nyingine ‘Tema Mate Tumchape’
Kupitia akaunti yake ya Instagram Madee ame-share cover ya single hiyo mpya iliyotengenezwa MJ Records.
Meneja wa Tip Top Connection Hamis Tale aka Bab Tale ameiambia Bongo61 kuwa wimbo huo utatoka rasmi Jumatatu ijayo (September 9).
No comments: