Baada ya kuachia video yake mpya iliyofanywa kwa gharama ya takribani milioni arobaini na tano za kitanzania, mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz amefananishwa na marehemu Steven kanumba kwa jinsi anavyothubutu kufanya mambo makubwa kukuza Sanaa na kipaji chake tofauti na wasanii wengine wenye majina makubwa nchini.
Hayo yameongelewa na Msanii dully sykes katika mahojiano yake na mtandao waBongo5 hii leo... Katika interview hiyo Dully amemuelezea marehemu kanumba kama ni mtu aliyethubutu kutumia nguvu, hali na mali, kwa ajili tuu ta kukuza jina lake kitu ambacho ni nadra sana kwa wasanii hasa wa Tanzania.
“Kanumba alikuwa ana uwezo wa hata kuchukua nauli yake ya kwenda sehemu kama Ghana kwenye tamasha la movie lakini ilimradi kujitengenezea status yake. Kwahiyo Diamond ni mtu ambaye tayari ameshajitolea kwaajili ya kuutetea muziki wetu.” Alisema Dully sykes
No comments: