Hivi karibuni tulimefanya mahojiano na mwanadada Wastara Sajuki ,pamoja na mambo mengi tuliyoongea naye moja lilikuwa ni kuhusu Filamu yake mpya ya Shaymaa inayotarajiwa kuingia sokoni kwa kasi hapo mapema mwezi ujao.
Katika interview hii fupi ya kutaka kujua ni nini mwanadada huyu anafanya kwa sasa Wastara amesema kwa sasa moyo wake, macho yake na akili yake ipo kwenye Filamu hii mpya anayotarajiwa kuitoa hapo mwezi wa kumi moja.
“Kwakweli kwa sasa siwazi ktu chochote, mawazo yangu yoote, akili, na nguvu zangu yapo juu ya SHAYAMAA, hii Filamu ni nzuri sana, kila nikiitazama nazidi kuipenda, sizani kama kuna Filamu kama hii kwa sasa” Alisema Wastara
Filamu hii amemshirikisha Yusuph Mlela na Nisha na amewataka fans wote wanaotaka kujua nini kimafanyika humo ndani kujipatia nakala zao mapema kwani copy zitakuwa chache sana.
(PICHA: Cover original za filamu hiyo)
No comments: