Inasemekana Mwanamke anapofikia umri wa miaka 25 huanza kujiuliza kuhusu kuolewa, lakini pia huanza kujiuliza kuhusu watoto. Kama hajaolewa, hana mchumba au anahisi kutokupata mtu anayeamini atamfaa, huanza kuhofia. Anapofikia umri huo huanza kujiuliza pia kuhusu watoto.
Hofu za maisha ya upweke ya baadaye humjaa na kumfanya kuanza kubabaika. Ni katika kubabaika huko, ndipo ambapo huweza kufanya mambo ambayo watu wengine hujiuliza ni kitu gani kimemsibu.
Kwa kuhofia kuchelewa kuolewa au kutoolewa kabisa, anaweza kumkubali mtu ambaye vinginevyo asingekubali kuwa naye kama mume. Kwa hofu ya kuingia kwenye umri mkubwa akiwa hana mume, humbeba yeyote.
Katika mazingira kama haya ndipo ambapo unakutana na wale ambao huolewa kwa madai ya kuondoa mkosi.
Anachotaka ni kuolewa na mwanaume yeyote, ili mradi ionekane kwamba, maishani mwake naye alishawahi kuolewa.
Kinadada mfunguke kama haya ni ya kweli ...
No comments: