» » » Linah afungua kampuni ya mavazi ‘Neyonce Designer’



Linah Sanga amesema amefungua kampuni ya mavazi iitwayo Neyonce Designer, ambayo itajihusisha zaidi na kushona na kubuni mavazi ya aina mbalimbali.
803454542ac511e3879322000a9f1376_7
Akizumgumza na Bongo5 leo akiwa mkoni Tanga kwaajili ya Serengeti Fiesta, Linah amesema kampuni hiyo ambayo imeshaanza kufanya kazi jijini Dar es salaam, tayari imeajiri vijana wawili na ina ofisi ya kudumu pamoja na mashine mbalimbali za shughuli za ushonaji.
“Tumefungua kampuni ya mavazi ambayo nimeshirikiana na binamu yangu ,itakuwa inajihusisha na shughuli za ubunifu wa mavazi mbalimbali, ushonaji pamoja na mambo mengine na lengo letu kuwa na kampuni kubwa ya ushonaji ambayo itakuwa na brand kubwa inayotambulika Tanzania nzima,” alisema Linah.
“Nataka kuacha na dhana ya kutegemea muziki peke yake kwasababu muziki una mwisho wake, inatakiwa wakati tuna uwezo wa kufungua kampuni ambazo zitatuongezea kipato ni vyema kufungua ili kuwa na uhakika wa vyanzo vingi vya mapato pamoja na kutoa ajira kwa wengine.”

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply