Hatimaye Ney Wa Mitego amepata nafasi ya kuhusika kama jaji wa Kitivo kwenye mashindano yanayoendelea hivi sasa ya Epiq Bongo Star Search 2013. Akiwa hana muda mrefu tangu aachie ngoma yake ya mwisho iitwayo ‘Salaamu Zao’, ngoma ambayo amewazungumzia watu maarufu wengi wengi akiwemo the big boss wa EBSS- Madam Ritha juu ya mwenendo wa mashindano hayo na washindi wake, Madam Ritha amempa shavu la kuwa jaji wa Kitivo kwa wiki ijayo.
“Ilikuwa ashiriki nafasi hiyo tangu wiki iliyopita lakini kutokana na ratiba zake kumbana ilishindikana, lakini kwa sasa kila kitu kipo sawa na wiki ijayo atakuwepo kwenye mashindano kama jaji wa Kitivo kinachoongozwa na mwalimu wa sauti wa washiriki. Kifupi hakuna tatizo.” – Madam Ritha ameiambia BK.
EBSS 2013 imefikia hatua ya kumi na mbili bora ambapo wiki ijayo kuna washiriki wawili wataaga mashindano hayo.
No comments: