Habari kwa Ufupi :

» » Pele kutoka Brazil azindua kitabu chake alichokipa jina la idadi ya magoli aliyofunga ’1283’

Legend wa soka kutoka Brazil Pele amezindua kitabu chake kipya ambacho kinajumuisha matukio mbalimbali ambayo ni kumbukumbu ya enzi zake alipokuwa mchezaji wa Brazil.



Kitabu hicho kinasemekana kuvunja rekodi ya uzito kwa kuwa na kilo 15, Pele amekipa jina la ‘1283’ ikimaanisha idadi ya magoli aliyowahi kufunga enzi zake za uchezaji.



Ni nakala 1283 tu za Kitabu hicho chenye jumla ya picha 500 zilizochapishwa.

Pele wakati wa enzi zake

Kitabu hicho cha Pele kilichozinduliwa huko Sao Paulo, Brazil kitapatikana kwa $1,700 sawa na shilingi 2,700,000/=.

Pele mwenye miaka 72 alisema picha zilizoko katika kitabu hicho zilikuwa ni za hisia sana kwake na zinamkumbusha watu wote waliompenda na kumsaidia katika kipindi alichokuwa mchezaji.

“It makes me think of all the people who loved and helped me during my career, my family, friends, the fans,”Alisema

Kitabu hicho kinategemewa kuingia sokoni Jumatatu ijayo katika maduka ya vitabu yaliyochaguliwa.

Source: Mail Online 

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Rose Ndauka Na Mpenzi Wake wategemea kupata mtoto ‘soon’
»
Previous
BEHIND THE SCENE: SUGUA GAGA YA SHAA NA DIRECTOR ADAM JUMA YAFANYIKA MAGOMENI... KAA TAYARI KWA VIDEO...

No comments:

Leave a Reply