
Mnyika aliongeza kuwa waraka huo uliochapisha kwenye baadhi ya magazeti na mitandao mbalimbali ya kijamii sio ule uliowahukumu wahusika hao na kuwaomba watanzania na wafuasi wa chama hicho kutoutilia maanani waraka huo na siku itakapobidi kuutoa waraka husika watafanya hivyo.
Akizungumzia mkutano uliofanywa na Zitto na wenzie licha ya kukata kusema hatua zitazozochukuliwa pindi watakaposhindwa kutimiza mashati waliyoyaweka, Mwanasheria mkuu wa chama hicho Tundu Lissu amesema mkutano huo ulilenga kupoteza lengo kuu la kuvuliwa madaraka na kuwa kilichowafukuza ni mkakati wao wa siri uliolenga kukipindua chama hicho na si vinginevyo.
Tundu Lissu aliongeza kuwa Zitto na wenzake hawajafukuzwa kwasababu ya taarifa za uongo za PAC,hawakufukuwa kwasababu ya posho,hawakufukuzwa kwasababu ya ya kuuza majimbo ya uchaguzi mwaka 2010,hawakufukuzwa kwaajili ya mambo mengine waliyoyataja bali wamefukuzwa kwa kuandaa mpango wa mapinduzi nje ya katiba ya chama, nje ya kanuni ya chama na nje ya namna ya kugombea uongozi nje ya chama.
No comments: