Yanga SC ilikuwa imepangwa Kundi C la michuano hiyo inayoanza kesho pamoja na Spice Star, Azam FC na Tusker ya Kenya- maana yake kwa kujitoa kwao, Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) kitalazimika kupanga upya Ratiba yake au kuiingiza timu nyingine katika nafasi ya mabingwa hao wa Bara.(P.T)
Mapema jana, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga SC, Mussa Katabaro aliiambia BIN ZUBEIRY kwamba wanachelewa kwenda Zanzibar kwa sababu hawajapata mwaliko na waliwaandikia barua ZFA juu ya hilo, lakini hadi sasa hawajapata majibu.
Wakati huo huo: Wachezaji wawili Waganda wa Yanga SC, Emmanuel Arnold Okwi na Hamisi Friday Kiiza waliotarajiwa kuwasili leo Dar es Salaam kutoka kwao, Kampala kujiunga na wenzao wamekuwa wakipigiwa simu tangu asubuhi, lakini hazipatikani.
Kizuguto amesema kwamba jana alizungumza na wachezaji hao na wakamthibitisha kwamba wanakuja leo, lakini kila akiwapigia simu hawapatikani.
Je, wako angani kwenye ndege wanakuja, au wamezima simu kuepuka usumbufu?
Ikumbukwe Yanga SC ilimfukuza kocha wake, Mholanzi, Ernie Brandts baada ya kufungwa mabao 3-1 na mahasimu wao, Simba SC katika mechi ya Nani Mtani Jembe Desemba 21, mwaka huu.
Pamoja na kumfukuza Mholanzi huyo, Yanga inataka kuwafukuza na Wasaidizi wake pia na tayari imekwishafikia makubaliano na Charles Boniface Mkwasa, awe kocha Msaidizi, nafasi ya Freddy Felix Minziro.
No comments: