» » Azam FC yaanza vyema CAF, yaifunga Ferroviario 1-0

IKICHEZA mchezo wa kimataifa kwenye uwanja wake wa nyumbani kwa mara ya kwanza katika historia yake AzamFC leo imepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ferroviario de Beira ya Msumbiji katika mchezo wa kwanza wa Raundi yaAwali Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam jioni hii.

Shukrani kwake mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Kipre Herman Tchetche aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 41baada ya kutengewa pande nzuri la kichwa na Mganda Brian Umony na kufumua shuti kali.



Mchezo ulikuwa mkali dakika zote 90 na mashambulizi yalikuwa ya pande zote mbili. Lakini Azam FC walitawalasehemu kubwa ya mchezo licha ya kushindwa kutumia nafasi nyingi walizotengeneza.

Mshambuliaji wa Ivory Coast, Kipre Tchetche na Mganda Umony kwa pamoja na Mzanzibari Khamis Mcha ‘Vialli’walitengeneza safu ya ushambuliaji iliyoanza lakini Mcha hakuwa kwenye kiwango chake kilichozoeleka nakuonekana kuwategea wenzake muda mwingi.

Refa Mutaz Abdelbasit Khairalla na wasaidizi wake Waleed Ahmed Ali na Aarif Hassan Eltom wote kutoka Sudanwalionekana kabisa kuwapendelea wageni katika maamuzi yao.

Dakika ya 70 beki mmoja wa Ferroviario aliunawa mpira wazi wazi kwenye eneo la hatari kufuatia shuti la KipreTchetche mbele ya refa, lakini akapeta.


Matokeo hayo yanamaanisha Azam itakuwa na kazi ngumu katika mchezo wa marudiano wiki mbili zijazo nchiniMsumbiji, wakitakiwa kulazimisha sare ama kushinda ili kusonga mbele.


Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ali, Erasto Nyoni, Malika Ndeule, Aggrey Morris, Said Mourad, Kipre Balou,Salum Abubakar, Himid Mao, Khamis Mcha/John Bocco dk61, Kipre Tchetche na Brian Umony/Jabir Aziz dk81.

Ferroviarrio; William Manyatera, Zefanis Matsinhe, Emidio Matsinhe, Abrao Cura/Kiki Simao, Edson Morais, ReinildoMandava, Valter Mandava/Hery Antony, Antonio Machava, Manuel Fernandes, Mario Sinamunda na ManuelCorreia/Dje Buzana.
 

Chanzo: Azam Fc 

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply