» » » Ben Pol katika Filamu mpya ya Sunshine,Kuingia sokoni Feb 20 2014

Pata kumuona Msanii  na Mkali wa R&b Ben Pol katika Filamau mpya ya Sunshine iliyofanywa na kampuni ya Karaban Film, ambapo ndani ya filamu hii utawakuta wakali kibao wa Bongo Movie Tanzania.

Katika Filamu hii ya  Sunshine aliyoigiza Ben Pol na Bi. Kiroboto itaingia sokoni February 30, 2014. Filamu zingine zitakazoingia sokoni tarahe hiyo ni pamoja na mdundiko na Network.


Hadithi ya Sunshine:


Lufu ni kijana msomi na mwenye hasira. Hakubaliki kazini kwasababu ya ulevi, madawa ya kulevya na wanawake ambao wamemsababishia matatizo mengi. Akiwa na miaka 22 tu tayari anatumia madawa ya kupunguza makali ya virusi vya ukimwi na kujiingiza kwenye maisha ya uhalifu mdogo mdogo.

Lufu anatoka kwenye familia nzuri na yenye upendo. mama yake, mama Eva ni mwanamke anayefanya kazi kwenye mgahawa kwa bidii na mtoto wake Eva.





Mama Eva anajua maisha ya Lufu yanategemea kula chakula chenye afya, na kuishi kwa kutumia dawa zake. Anawasiwasi kuhusu mtoto wake na dhiki inamuua.

Wakati Mama Eva amezimia na kushauriwa kwamba anahitaji upasuaji wa moyo wakati familia yake ni duni. Lufu anaamua kuliweka jambo hili mikononi mwake mwenyewe. Afanye nini ili apate fedha kwa ajili ya mahitaji ya familia na kuokoa maisha mama yake.

Pindi filamu hii itakapotoka jaribu kuitafuta na utakutana na Hadithi ya upendo kati ya mama na mtoto wake.

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply