Mwanamuziki na muigizaji baby Joseph madaha amefunguka na kusema kuwa kweli ameamini uchawi na kupigana juju vipo kwenye gemu kwani mambo yaliyomtokea hivi karibuni haelewi hata imekauje.
Baby Madaha ambaye amerudi nchini hivi karibuni tokea Nairobi alipoenda “ku-solve” ishu yake hiyo na label hiyo anasema yani hata haelewi kitu gani kilitokea siku hiyo ingawa mpaka akaandikwa kama alienda kujiuza, anachokumbuka ni kupigiwa simu na mtu asiyemfahamu an kumwambia anataka wafanye naye kazi ya kusambaza filamu yake mpya ya Gal Bladder ambaye inatikisa soko kwa sasa.
Baada ya kufika hapo waliongea vizuri na kuondoka ghafla kabla ya kuja kusoma kesho yake kuwa alikuwa anajiuza kitu ambacho ansema hajui kimetoka wapi.
“Yani hata sielewi ilikuaje nikaenda kukutana na yule jamaa, ilikuwa ni kama muujiza hivi, mwanzo nilisita sana ila nikashangaa nimefika tu pale bila kujielewa, ni vitu vya ajabu sana” alieleza baby Madaha.
Chanzo nini?
Hapo siku za nyuma baby Madaha alipatikana na dhahama ya kukumbwa na kashfa nzito sana ya kujiuza kwa dau la milioni kumi kwa jamaa mmoja hivi mitaa ya Dar es Salaam Jambo lilolopelekea yeye kupigwa chini na Record label yake ya Candy and Candy ya huko Kenya na kupokonywa gari aina ya AUDI TT aliyokuwa akitembelea huku akiharibu pia uhusiano wake na bosi wa record label hiyo - Joe kairuki ambaye pia anadaiwa kuwa mpenzi wake.Je ni Kweli alijiuza?
Baby Madaha ambaye amerudi nchini hivi karibuni tokea Nairobi alipoenda “ku-solve” ishu yake hiyo na label hiyo anasema yani hata haelewi kitu gani kilitokea siku hiyo ingawa mpaka akaandikwa kama alienda kujiuza, anachokumbuka ni kupigiwa simu na mtu asiyemfahamu an kumwambia anataka wafanye naye kazi ya kusambaza filamu yake mpya ya Gal Bladder ambaye inatikisa soko kwa sasa.
Baada ya kufika hapo waliongea vizuri na kuondoka ghafla kabla ya kuja kusoma kesho yake kuwa alikuwa anajiuza kitu ambacho ansema hajui kimetoka wapi.
“Yani hata sielewi ilikuaje nikaenda kukutana na yule jamaa, ilikuwa ni kama muujiza hivi, mwanzo nilisita sana ila nikashangaa nimefika tu pale bila kujielewa, ni vitu vya ajabu sana” alieleza baby Madaha.
Uhusiano wake na Label hiyo ukoje sasa?
Baby amesema kwa sasa kila kitu kipo sawa kwani alipoenda Kenya waliongea vizuri na bosi wake huyo na kumaliza tofauti zao na sasa amerudi nchini kusambaza filamu yake hiyo mpya ya Gal bladder huku akijiindaa kupiga show kwenye tour yake aliyoiandaa jina la Top Up and Refill itakayofanyika mwezi ujao wa tatu.Mwenyewe anasemaje zaidi?
Hata wafanyaje, waniroge, wanichafue, i'm a bad gal, na sibabaishi na vijimaneno vya watu hata kidogo, sitoki candy and Candy hata waloge kwa waganga wote duniani. Kama walifikiri nimeumbuka, wajue watasubiri sana. Nikitoka kenya naenda Holywood tu!
No comments: