Kuna wengi wamemmiss ray c na ni muda mrefu sasa umepita game la bongo flavor limemkosa msanii wa kike hit maker wa ‘Uko Wapi’ Ray C, ambaye alijipatia umaarufu mkubwa si tu Tanzania bali hata nje ya mipaka, kutokana na sauti yake pamoja na ukataji mauno awapo jukwaani.
Ray C
Ray C ambaye jina lake halisi ni Rehema Chalamila, ameahidi kurudi kazini (kwenye muziki) muda si mrefu sababu hata yeye ameimiss mic na jukwaa, “Naimiss steji vibaya mno!!!!” ameandika Ray C katika Instagram yake.
“Likizo ya mwaka mzima alhamdullilah!!!!Mungu ni mwema sana!!!!!!!Asante kwa afya baba yangu!!!!!muda si mrefu ntarudi Kazini na uhakika mashabiki wangu wapenzi mmenimiss sana!Kila kitu tayari kimeshapikwa bado tu kuwaambia lini tu but niombeeni heri wapenzi wangu najua sana mmeimiss sauti ya Ray C All over the world!!!!jinsi ninavyowapenda na jinsi mlivyoniombea zawadi Kama kumi hivi nimewaandalia!!!mtashauaje sasa!!kama nawaona vile!!!!!!Bila nyie hakuna Ray C!!!!!!!Thank you so very much guys!!!!!!My fans!My everything!!Nawapenda mno!!!!”.
Mwishoni mwa mwaka jana Ray C alisema ameanza kuingia studio na tayari amemaliza kurecord album yake mpya, hivyo naamini comeback yake itakata kiu ya mashabiki wake.
No comments: