» » » Mama wa Kim Kardashian awataka Kanye west na Kim Waondoke Kwake

Mama yake na Kim Kardashian, Kris Jenner anadaiwa kumtaka binti yake huyo pamoja na mchumba wake Kanye West waondoke nyumbani kwake.



Kim akiwa na mama yake

Ni Kris ndiye aliyemwalika Kim wakae pamoja baada ya mrembo huyo kujifungua mtoto wake, North West, June 2013, kwakuwa nyumba yao ya Bel Air ilikuwa bado ikiendelea kujengwa.



Lakini kwa sasa mwanamke huyo mwenye miaka 58 amechoka kujisikia kama mgeni kwenye nyumba yake mwenyewe na inadaiwa kuwa alimpigia simu mhandisi wa nyumba ya Kim kwa siri kumwambia akaze mkono amalize nyumba hiyo ili mwanae aondoke.

Kanye West akiwa na Mama Watoto wake Kim Kardashian

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply