» » Klabu Ya Soka Azam Yaelekea Msumbiji Jana Kuikabili Ferroviario de Beira

Msafara wa watu 37 wa klabu ya soka ya Azam leo umeelekea mjini Beira nchini Msumbiji, kuikabili Ferroviario de Beira katika mechi ya pili ya raundi ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Picha za Timu ya AZAM wakiwa uwanja wa ndege kabla ya safari yao kuelekea mjini Beira nchini Msumbiji.





Azam FC itarudiana na timu hiyo ya Msumbiji, Jumamosi wiki hii baada ya kuwa timu hizo zilimenyana juzi Jumapili kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na wenyeji kushinda kwa bao 1-0. Bao hilo lilifungwa na nyota wa Ivory Coast, Kipre Tchetche. Ili kusonga mbele katika hatua ya kwanza, vijana hao wa Joseph Omog, watapaswa kuhakikisha hawafungwi, badala yake wapate sare ya aina yoyote au ushindi.



Kwa mujibu wa Meneja wa Azam FC, Jemedari Said, kikosi cha timu hiyo kitakuwa na wachezaji 21 na viongozi 16 wakiwamo wa benchi la ufundi na viongozi wa klabu hiyo inayoshiriki michuano hiyo kwa mwaka wa pili mfululizo.



Wachezaji waliyounda kikosi hicho kilichosafiri leo ni Mwadini Ali, Aishi Manula, Jackson Wandwi, Erasto Nyoni, Malika Ndeule, Luckson Kakolaki, Aggrey Morris, Said Morad, Kipre Bolou, Ibrahim Mwaipopo, Jabir Aziz na Himid Mao.

Wengine ni Salum Abubakar, Seif Abdallah, Kipre Tchetche, Brian Umony, Kone Ismail, Gaudence Mwaikimba, Mcha Khamis Mcha, David Mwantika na John Bocco.

Na hili ndio benchi la ufundi linaloundwa na Kocha Mkuu Omog, raia wa Cameroon, makocha wasaidizi, Kally Ongalla na Ibrahim Shikanda, Kocha wa Vijana, Idd Cheche, Daktari Juma Mwankemwa, Daktari wa viungo Vicent Madege na Mtunza Vifaa Yussuf Nzawila.

Wengine ni Katibu Mkuu wa klabu, Idrisa Nassoro, Ofisa wa Itifaki, Abubakar Mapwisa, Jamal Bakhresa, Msemaji wa Azam Media, Florian Kaijage na Jaffar Maganga na Kassim Khan pia kutoka Azam Media.

Credit:AzamFcWeb

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply