Gazeti hilo limeendelea kuandika kuwa wiki hii Rais Jakaya Kikwete, atakutana na Prince of Wales, Duke of Cambridge, Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron na Rais mambo ya nje wa nchi hiyo, William Hague kwenye mkutano wa viongozi wa nchi 50 huku Tanzania ikiwa na sifa mbaya kwa mauaji ya Tembo.
Mkutano huo ni mahsusi kwaajili ya kuokoa viumbe hao wanaohatarishwa kupotea kutokana na kushamiri kwa mauaji.
Mkutano huo wa Alhamis hii utajaribu kufikia muafaka kuhusiana na muitikio wa kidunia dhidi ya biashara haramu ya pembe za ndovu yenye thamani ya paundi bilioni 6 kwa mwaka na ambayo hudhamini makundi ya kigaidi.
Theluthi ya pembe zote za ndovu zinazokamatwa barani Asia hupitia Tanzania na kila siku tembo 30 huuliwa ambao ni sawa na tembo 11,000 kila mwaka.
No comments: