
Endelea kupata Habari Zaidi Kila siku Kutoka BONGO61.COM Kwa Kijiunga Hapa Buree!.
George Zimmerman

Zimmerman ndiye aliyependekeza kuwa na pambano la ngumi na staa yeyote.
Pambano hilo limeandaliwa na promoter maarufu, Damon Feldman wa kampuni ya Celebrity Boxing. Wiki iliyopita alisema alikuwa anakubali ombi la mtu yeyote atakayependa kupanda ulingoni kupambana na Zimmerman katika pambano litakalooneshwa kwa kulipia.
“Habari hiyo ina saa moja tu e-mail yangu imejaa zaidi ya watu 8,000 wanaotaka kuchuana na George, ” Feldman aliiambia CNN wiki iliyopita.
Mapema Jumatano hii amesema amemchagua mshindani. Katika maombi zaidi 15,000 yaliyotumwa kwa e-mail, amesema amemchagua DMX. Tarehe, muda na sehemu ya pambano hilo itatangaza Jumatano ijayo.
No comments: