» » » » Picha: Godwin Gondwe a.k.a ‘Double G’ ajiunga na Clouds FM/TV?

Baadhi ya wafanyakazi wa Clouds Media Group wiki hii walikuwa ‘chimboni’ jijini Arusha ambako walienda kutengeneza mikakati ya namna ya kuingia kwa nguvu kwenye jukwaa jipya la utengenezaji wa ‘content’ kwenye mfumo wa dijitali zaidi.


Watangazaji wa Clouds FM wakiwa Arusha

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Joseph Kusaga akielezea kuingia kwenye mfumo uitwao ‘Over the Top’ OTT so nahisi ziara hiyo ya Arusha ilikuwa ni kwaajili ya kujipanga zaidi.

Vijana hao wanarejea Dar es Salaam kuendelea na majukumu yao ya kila siku but guess what (kwa sauti ya Dee Andy).. inaonekana mtangazaji mkongwe aliyewaHi kutangaza Radio One, RFA na sasa akiwa msomaji wa habari wa ITV, Godwin Godwin aliungana na vijana wa mjengoni jijini Arusha.




Kutoka Kushoto: Millard Ayo, Mbwiga wa mbaaaali, Perfect Crispin, Gerald Hando na Godwin GondweGodwin ameonekana na watangazaji hao wakiwa kwenye uwanja ndege wa Arusha kurejea Dar.




Kutoka Kushoto: Mbwiga, Millard Ayo, Perfect Crispin, Gerald Hando na Godwin Gondwe (huyo mwingine sijui nani!!)

Picha hiyo inazalisha maswali mengi iwapo Double G ameungana na Clouds Media Group ama ni abiria tu kwenye ndege hiyo na aliamua kupiga picha nao…

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply