» » » Sheddy Clever: kupitia My Number 1 ya Diamond Platnumz Nimejifunza na kupata changamoto nyingi.

Mtayarishaji wa muziki kutoka studio za Burn Records, Shedy Clever amesema chanagamoto alizokutana nazo wakati akifanya kazi na mwanamuziki the super star wa Bongo Flavour Diamond  Platnumz zimemfanya aifunze mambo mengi.

Sheddy Clever aliyetengeneza wimbo wa My Number 1 wa  mwanamuziki Diamond Platnumz amesema kufanya kazi na nyota huyo kumemfunza vitu vingi katika muziki, baada ya kutengeza kazi za wasanii wengine wakubwa.

Sheddy Clever

"Nimefanya kazi na wasanii wengi wakubwa na wadogo na mara nyingi wao huwa wakinisikiliza mimi kama producer lakini nilipofanya kazi na Diamond alikuwa akinielekeza na kutaka kushirikiana pamoja katika kutengeneza kazi hiyo, kuna wakati aliniambia kitu flani kimekosewa, hiki akipo sawa na kweli nikisikiliza kwa makini nagundua hilo na hii yote ni kwa sababu Diamond Platnumz anapenda kazi yake na yupo makini na kazi yake" Alisema Producer Sheddy Clever

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply