Ndege ya Malaysia Airlines iliyokuwa na abiria 227 na wafanyakazi 12 inahofiwa kuanguka huko katika bahari kusini mwa China, kwa mujibu wa shirika la habari la serikali la Vietnam.
Ndege ya Malaysia Airlines Boeing 777-200ER
Ndugu wa abiria waliokuwa kwenye ndege hiyo wakisubiri taarifa kuhusiana na ndege hiyo
Ndege hiyo aina ya Boeing 777-200ER iliyokuwa inatoka Kuala Lumpur kuelekea Beijing, ilikuwa imepotea kwa masaa kadhaa. Kama ripoti hiyo ikithibitisha, itakuwa ni ajali mbaya ya ndege ya aina hiyo (Boeing 777) tangu iingie sokoni miaka 19 iliyopita.
Ndugu wakifanya mawasiliano kutaka kujua ukweli
Malaysia Airlines bado haijathibitisha iwapo ndege hiyo imeanguka.
Malaysia Airlines bado haijathibitisha iwapo ndege hiyo imeanguka.
No comments: