Desire baada ya kitendo hiki, amesema kuwa ameweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza Uganda kununua gari wiki 5 kabla ya kufanya onesho binafsi, ikiwa ni ishara ya kuwa onesho analokwenda kufanya si kwa madhumuni ya kujitengenezea pesa kama faida, bali ni kwa ajili ya kuburudisha mashabiki.
Desire pia amefanikiwa kujiweka katika nafasi nzuri zaidi hasa baada ya kupata wadhamini watakaosimamia sehemu kubwa ya gharama za onyesho, ingawa mwanzoni suala hili lilizua wasi wasi kutokana na wadhamini kuchelewa sana kujitokeza.
No comments: