Habari kwa Ufupi :

» » » Diamond alilia wakati akifanya Chorus ya Kipi Sijasikia 'Profesa Jay'

Hit maker wa Kipi sijasikia Profesa J amesema Diamond Platnumz, alilia machozi wakati anafanya chorus ya wimbo wake ‘Kipi Sijasikia’



Rapper huyo alikiambia kipindi cha Sunrise cha Times FM kuwa wakati Diamond anarekodi chorus hiyo yeye na Majani walishangaa kumuona hitmaker huyo wa ‘My Number One’ akibubijikwa na machozi ndani ya ‘booth’.

“Lakini kilichotushangaza alipoingia booth ili arekodi chorus Diamond alikuwa anaimba huku analia. Sisi tuko kwenye monitors huku tunamuangalia jamaa upande wa pili kwenye booth tunamuona Diamond analia. Alikuwa emotional unajua ile…ilimgusa sana. Sisi tulikuwa tunashangaa mimi na Majani ‘huyu jamaa analia nini?’ Lakini baadae tulimuuliza alituambia ‘nimefurahi sana katika maisha yangu kufanya kazi na Profesa Jay pamoja na Majani, hilo moja. Lakini pili, mlivyoimba humu ndani vyote vinanihusu mimi…vimenitokea sana katika maisha yangu na changamoto zote hizo’..so yale ndio yalitokea studio. Kiukweli hii ngoma ilikuwa blessed tangu studio na kila mtu alikuwa anasema ‘yeah men it’s on’, alisema Profesa J.
Source:Time Fm

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Music:Tanzania All Stars - Muungano
»
Previous
Mary Okoye 'Mdogo wao P-Square' avishwa pete ya uchumba na Muigizaji wa Nolywood

No comments:

Leave a Reply