Habari kwa Ufupi :

    3:00 PM
» » » Videos: Wagosi wa Kaya watoa video mbili mpya, 'Bao' pamoja na 'Gahawa'

Kundi la Wagosi wa Kaya toka Tanga wamerejea tena baada ya ukimya wa miaka nane na tayari wana albam mpya mkononi walioipa jina la ‘Uamsho’.

Kundi hilo linaloundwa na Mkoloni na Dr. John limeachia nyimbo mbili sambamba na video zake, nyimbo hizo ni ‘Gahawa’ na ‘Bao’.


Nyimbo hizo zilitambulishwa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha Bongo Dot Home cha 100.5 Times Fm Jumamosi iliyopita.

“Mfano watu wanajua Wagosi wa Kaya wao wakija ni siasa kwenda mbele tu hapana, sisi tumeshaimba vitu vingi sana. Tumeshaimba Wauguzi, tumeshaimba Soka la Bongo, Trafiki, Ubia, kilimo, tumeshaingia kila kona, zile nyimbo zipo tu na huu ni uamsho na albam yetu inakuja inaitwa ‘Uamsho’. Tunaamsha.” Wagosi wa Kaya waliiambia Bongo Dot Home ya Times Fm.

Zitazame hapa chini video zote mbili

1:Video Wagosi wa Kaya - Bao




2:Video Wagosi wa Kaya - Gahawa



Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Magazetini leo Jumanne ya Tarehe 15/4/2014
»
Previous
Rais huyu kutoka afrika atoa zawadi za iPhone za Gold katika harusi ya Binti yake

No comments:

Leave a Reply