» » Msichana mwingine wa kitanzania afariki kwa hii biashara nchini India

Ikiwa bado serikali inajipanga kupunguza human trafficking, huko nje mambo yanaendelea kuwa mabaya kwani mtanzania wa pili amefariki. Wa kwanza alifariki huko China na huyu wa pili anefariki nchini India katika jiji la New delhi. Mrembo huyo anaeishi tabata anaeitwa Neema Katabwa aliamua kwenda india kujitaftia maisha na baada ya kufika nchini India ndio akaanza biashara hiyo ya ukahaba mpaka pale alipokutana na mnigeria anaeitwa Akuba na kuamua kumuweka ndani.



Neema aliamua kukaa na Mnigeria huyo mpaka pale mauti yalipomkuta kwani source inasema mnigeria huyo hakujua kama Neema bado aliendelea na kazi yake ya ukahaba mpaka pale alipomkuta na ndio matatizo yalipotokea.Inasemekana  mnigeria huyo alimpiga sana mpaka hali yake kuwa mbaya na kuweza kukimbizwa hospitali mpaka mauti kumkuta. Kwa sasa ameletwa nchini kwa ajili ya mazishi lakini source inasema kuna rafiki yake anaeitwa Mercy anajua exactly kilichomkuta Neema huko New Delhi.
Kwa kweli hili sula la dada zetu kufanya biashara haramu limezidi kukithiri kila tukiamka na wanaopeleka dada zetu huko wanajulikana kwani huwa wanawapeleka kwa mkopo na mtu anahitajika kufanya biashara hiyo mpaka alipe deni la dola 35000 au hapewi passport yake.

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply