Mtangazaji wa kipindi cha Wanawake Live, Joyce kiria amefunguka ya moyoni na kumpa pole mwanamuziki wa zamani na mbunge Vicky Kamata baada ya ndoa yake kudaiwa kuzuiliwa kufungwa baada ya kubainika kuwa mwanaume aliyetaka kufunga ndoa naye ana ndoa nyingine ya kanisa.
Vicky Kamata akiwa hospital
Kupitia Facebook, Joyce ameandika haya:
Hii habari imenihuzunisha sana. Ninachoweza kusema ni kwamba (1) Tuwe waaminifu kwenye mahusiano tuliyonayo. (2) Endapo tumeshindwa kuelewana au kuishi pamoja basi tumalizane kiutu uzima au kistarabu kila mtu achukue 50 zake kwa Amani. (3) Tusikomoane pale mtu anapoanza maisha yake mengine na mtu mwingine. Tatizo lipo kwa wahusika Hasa hasa suala la “Uaminifu” au suala la “kukomoana”, Kanisa limesimama kwa nafasi yake. Mh Vicky kama hili tukio ndo sababu ya kuumwa kwako, nakupa pole sana, yaliyokukuta ni sehemu ya Maisha, usiumie kiasi cha kuhatarisha uhai wako. Wewe mshukuru Mungu kwa kila jambo. Mungu akupe wepesi kwa jambo hili mengine yatajiseti mbele kwa mbele….jamani tumuombee maana mahusiano ya siku hizi ni hatari tupu! Yasipokukuta wewe yanaweza kumkuta mwanao!! Usijione wewe ni mjanja sanaaaa ila mshukuru Mungu.”
Habari zimedai kuwa sababu zilizofanya ndoa hiyo isifungwe ni kutokana ni mwanaume aliyetaka kufunga ndoa na Vicky kuwa na ndoa nyingine ya kanisa na amejaaliwa kupata watoto kadhaa hivyo isingekuwa rahisi kufungwa kwa ndoa nyingine kwa mujibu wa taratibu za kidini.
Kwa mujibu wa Global Publisher, mwanaume huyo alishatoa mahari kwa msichana mmoja wa jijini Dar na ukweni anajulikana, na ya mwisho ni Vicky aliugua ghafla na kulazwa katika Hospitali ya Tabata General jijini Dar kwahiyo isingekuwa rahisi ndoa kufungwa Jumamosi kutokana na hali yake kuwa mbaya
No comments: