» » Justin Bieber na Selena Gomez mapenzi tele

Justin Bieber na Selena Gomez ambao walikuwa wamepigana kibuti wameamua kuuyarudisha mapenzi yao kama zamani.

Wawili hao wameonekana maeneo ya Los Angeles wakiwa wanaendesha kigari cha matairi matatu na walihudhuria pamoja sherehe ya siku ya kuzaliwa ya rafiki yao Alfredo Flore Jumatatu, June 16, 2014.



“Justin na Selena wamerudisha mapenzi yao kabisa na wako pamoja muda huu. Walitumia siku nzima wakiwa pamoja…Justin alikuwa anaendesha wakati Selena akiwa amekaa nyuma ya Kigali hicho akiwa amemshikilia.” Chanzo kimeiambia US Magazine.

Mtu wa karibu wa Justin na Selena alieleza kuwa bado story iko vilevile, leo wataonekana wako vizuri ila wiki ijayo watagombana tena na kuachana.

“Hawajawahi kuacha kuongea hata kama huwaoni pamoja. Wanagombana, wanapumzika na baadae wanarudi tena pamoja.” Alisema.

Justin Bieber aliwafanya watu waamini kuwa wamerudiana na Selena baada ya kupost picha kwenye Instagram akiwa na Selena nakuandika, “Our Love is unconditional. ” lakini aliifuta picha hiyo baada ya muda mchache.

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply