» » » Justin Bieber, Apata wakati mgumu baada ya Majirani wa anapotaka kuhamia huko atlanta kupanga kuandamana

Ule ukorofi wa Justin Bieber sasa unapelekea awe tishio la watu wengi hususani wazazi ambao wanaogopa kuwa kwake karibu na watoto wao anaweza kupelekea kuwaharibu kitabia.



Mwimbaji huyo wa Canada Bieber (19) anatarajia kuhamia makazi mapya huko Atlanta alipopanga kwenye nyumba ya rapper Dallas Austin, na badala ya majirani kufurahia kupata jirani star, wamepanga kuandamana kupinga Bieber kuhamia eneo lao sababu wanahofu anaweza kuwaambukiza tabia mbaya watoto wao.

Kwa mujibu wa TMZ wakazi hao wa Buckhead, Atlanta wamepanga kuandamana leo Jumatatu, na zaidi ya wakati 200 wa eneo hilo wamethibitisha kushiriki kwa kusaini ‘petition’ inayosomeka:

“Tumefanya kazi kubwa kufikia malengo yetu na kufika hapa tulipo, kuhamia kwa Justin Bieber Atlanta ni mbaya kwa watoto wetu. Wengine wanashindwa kuwaacha watoto wacheze bila uwogo, amekuwa akikimbiza magari hapo nyuma…Tafadhali usiruhusu mtoto aharibu tulichofanyia kazi kwa bidii kukipata”.

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply