Nyaisangah alikuwa Meneja wa kituo cha radio cha Abood FM pamoja na Abood TV cha mjini Morogoro.
“Kaenda hospitali jana mchana saa nane na amefariki leo Alfajiri lakini kabla ya hapo alikuwa akienda hospitali kupata matibabu na kuweza kurudi,” amesema Dogoli. “Mipango ya mazishi tunasubiri ndugu walioko Dar es Salaam, walioko Tarime ili wakae kama familia wapange msiba utakuwa wapi.”
Akimuongelea, Nyaisangah aliyewahi pia kuwa mtangazaji wa Radio One, Dogoli amesema Nyaisangah hakuwa tu meneja wa kituo hicho cha radio, bali alikuwa kama mwalimu wa watangazaji na pengo lake haliwezi kuzibika.
“Alikuwa na mtu wa msaada mkubwa kama unavyomfahamu ni mtu unique, ana vitu ambavyo wengine hawana na aliweza kuwabadilisha wafanyakazi wa Abood Media na wakafika sasa kuwa katika hali ya ubora. Kifo chake kimetuhuzunisha sana, kila mtu ameguswa na pengo lake litachukua muda kuweza kupata mtu kuliziba. Kupata mtu wa aina yake itachukua muda.”
Mungu ailize roho yake mahala pema poponi.
No comments: