Maelezo yaliyoandikwa kwa mkono kwenye kurasa 9 na mwanamke anayetafutwa na kuvuma zaidi duniani, Samantha Lewthwaite aka ‘White widow’ yameonesha jinsi alivyonuia kupandikiza chuki na visasi wa kigaidi kwa wanae.
Magaidi wa baadaye? Samantha Lewthwaite aliandika kuwa anawaandaa wanae, (pichani) kuja kuwa magaidi kama baba yao
Karatasi hizo zenye maandishi ,zilipatikana kwenye nyumba aliyokuwa akiishi nchini Kenya ambapo yeye na wanakarakati wengine wa kiislamu walikuwa wamepanga kushambulia hoteli mbili na kituo kikubwa cha manunuzi,.
Hii ni Nyumba ya Kenya ambayo Samantha anadaiwa alikuwa akiishi
Polisi pia waligundua risasi za AK-47 na picha za watoto wanne wa mwanamke huyo. Karatasi hizo zimeonesha kuwa anakuza watoto hao wafuate nyayo za baba yao, Germaine Lindsay aliyejitoa mhanga na kuua watu jijini London.
Watoto wake wadogo, Abdur-Rahman mwenye miaka mitano na Surajah, 3, ni watoto wa gaidi aliyezaliwa London, Habib Saleh Ghani. Lewthwaite anatuhumiwa kupanga mashambulio kwenye maeneo ya Kenya yenye watalii wengi.
Mwanamke huyo aliyebadilisha dini na kuwa muislamu, anakisiwa pia kuhusika kwenye shambulio la mwezi uliopita kwenye jengo la Westgate jijini Nairobi ambapo watu 67 waliuawa. Watoto wake aliozaa na Lindsay, Abdullah, 9 na Ruqayyah, 8, wana majina ya kati Shaheed na Shahidah.
Lewthwaite alikuwa na ujauzito Ruqayyah kipindi Lindsay alipojilipua. Inadaiwa kuwa alikuwa amejificha nchini Tanzania au Somalia. Kwenye maelezo hayo, mwanamke huyo anaeleza jinsi alivyobarikiwa kuwa na mwanaume mgambo na jinsi alivyojitolea kuyaacha maisha ya raha kupigana na wasio waislamu.
Source: DAILY MAIL
No comments: