Rihanna amejikuta kikaangoni tena wiki hii baada ya mashabiki wake kumshambulia kutokana na video yake mpya ya wimbo ‘Pour It Up’ wakisema ni chafu na ina matusi mno.
Mamia walitumia mitandao ya kijamii kumponda mrembo huyo kwamba ‘hana hata haya’ kutoa video chafu kama hiyo. Walihoji kama kweli anaweza kuwa mfano wa kuigwa kwa mamilioni ya mashabiki wake vijana duniani.
Wanaharakati pia wameuomba mtandao wa YouTube kuipiga chini video hiyo ambayo hadi sasa imeshaangaliwa kwa zaidi ya mara milioni 16 tangu itoke Jumatano ya wiki hii. Wengine wamewataka wazazi kuwazuia watoto wasiitazame video hiyo.
No comments: