» » Serikali ya Kenya yatenga zaidi billion 5 za kuwakopesha wasanii wa muziki



Wakati wasanii wa Tanzania bado wanaililia Serikali kuweka mkono wake katika kusimamia biashara ya kazi za sanaa ili iwanufaishe, Serikali ya majirani zetu Kenya imeliona hilo na kuamua kutenga kiasi cha shilingi milioni 300 za Kenya sawa na zaidi ya bilioni 5 za Tanzania, kwaajili ya kuwawezesha wasanii kukopa fedha za kuwasaidia kuendeleza kazi zao za muziki.



Kwa mujibu wa Pulse, mwenyekiti wa mfuko wa maendeleo ya vijana Evans Gor Semelang’o amesema lengo la serikali ya Kenya ni kutaka kuwapunguzia mzigo wasanii ambao wanaupata wakati wa kuandaa kazi zao, hivyo imefanya hivyo kuonesha mchango wake katika kutimiza ndoto za wasanii hao ili kuleta utofauti na kukuza uchumi wa nchi.

Watakaonufaika na mfuko huo ni pamoja na waandishi wa nyimbo, dancers, waimbaji, rappers maproducer, mapromoter na wengine.

Ameongeza kuwa serikali inahitaji kila kijana mwenye kipaji cha muziki kutengeneza pesa kupitia muziki na kuleta mapinduzi ya muziki yanayohitajika.

SOURCE: PULSE

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply