» » Video na Picha: Majina ya magaidi 4 walioshambulia Westgate yatajwa, na video inayowaonesha wakiwa ndani ya jengo hilo yapatikana


Video mpya inayowaonesha magaidi walioshambulia Westgate wakiwa ndani ya store mojawapo ya maduka ndani ya jengo la Westgate jijini Nairobi wakati wa shambulio la (September 21).


Video hiyo iliyorekodiwa na camera za ndani ya jengo hilo ‘ CCTV’ inawaonesha magaidi wanne wakizunguka katika chumba hicho huku wakiwa wamebeba silaha nzito, na wengi wao wakiwa wamejifunga vitambaa vyeusi vichwani mwao.
Magaidi hao wanaonekana wakiingia na kutoka katika vyumba vya karibu na chumba walipo kama watu wanaokagua kitu.




Kwa mujibu wa Mail Online, msemaji wa jeshi la Kenya amethibitisha majina ya magaidi 4 wanaohusishwa na tukio hilo lililodumu kwa siku nne na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 60.

Major Emmanuel Chirchir wa Kenya ameyataja majina ya magaidi hao kuwa ni Abu Baara al-Sudani, Omar Nabhan, Khattab al-Kene and Umayr, majina ambayo yalitangazwa na vituo vya TV vya Kenya.

Alitweet ujumbe kwenda kwa shirika la habari la ‘The Associated Press’. “I confirm those are the names of the terrorist”.

Tazama video hiyo inayowaonesha magaidi hao wakiwa wanazunguka na silaha ndani ya chumba cha Westgate




Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply