» » Zingatia haya wakati unafanya Mawasiliano na mtu.

Je wajua kuwasiliana na watu ni zaidi ya kuongea? Watu wengi wanajua kuongea na watu ila hawajui kuwasiliana na watu. Mawasiliano ni jambo la muhimu sana hasa unapokua eneo la kazi na jamii ya watu wanaokuzunguka, hivyo inahitaji umakini mkubwa kwa kila neno linalokutoka kinywani. hivyo basi kuna vitu vya msingi unavyotakiwa kujua unapowasiliana na watu hasa kazini.




Pangilia mazungumzo yako

Unapokwenda kuongea na mtu au kutoa ripoti ya jambo fulani jitahidi kupangilia maneno, tukio na mtiririko wake ili kupunguza maswali kwa yule anaye kusikiliza. Chagua maneno ya kutumia, namna utakavyoanza maongezi na mifano utakayotumia kama inaendana na kile unachotaka kuwasilisha. Usikurupuke kwani unahatarisha kazi na taaluma yako.

Chagua lugha utakayotumia

Usijisikie aibu kuona kwamba watu watakuona hujui lugha fulani unapowasilisha kitu fulani. Kama hujachaguliwa lugha ya kutumia, tumia lugha unayoijua vizuri na ambayo unahisi utaeleweka vizuri wakati wa kuwasilisha mada yako.

Jaribu kujua utu wa mtu na Hulka yake

Watu wengi hupenda kuongea tu bila kujua mtu anayeongea naye ni wa namna gani na lugha gani au maneno gani atumie. Kuna watu ambao hawapendi maneno mengi hivyo ukimwendea na maneno mengi anashindwa kukuelewa na unakuwa unapoteza muda wake, anachokihitaji ni maelezo ya msingi katika kile unachokiongea. Usipende kuongea kila kitu kwa kila mtu, chukua nafasi ya kujifunza hulka za watu na tabia zao na za kwako pia ili uboreshe mawasiliano na watu wengine.

Tambua mawasiliano ambayo mtu anapenda kuyatumia

Katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia, namna watu wanavyowasiliana ni tofauti na zamani, hivyo unahitaji kuwa mbunifu na mtu unayeweza kujifunza haraka mabadiriko yanayoendelea. Si watu wote wanaopenda kupigiwa simu ama kila siku kumfuata ofisini kwake kama unamazungumzo naye. Kazi yako ni kujua wajibu wa kazi yako, nini unachotakiwa kukifanya ukifanye na ujue ,Bosi wako anapenda umpe mrejesho kwa mawasiliano gani ili kupunguza usumbufu katika utendaji na utekelezaji wa majukumu yenu.

Zungumzia kitu unachokijua vizuri

Unapowasiliana na mtu jitahidi kuwa mkweli na kujua unachokizungumzia vizuri na kwa undani wake, hiyo inakuongezea uaminifu katika eneo lako la kazi. kitu kama una uhakika nacho, omba muda zaidi wa kukichunguza kabla ya kutoa maelezo yako.

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply