Awali Rooney alikuwa amepa nga kuondoka mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kutofautiana na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Sir Alex Ferguson. Mabingwa hao wa ligi Kuu ya England walilazimika kupambana na ofa ya dau la £ milioni 30 kutoka Chelsea
Moyes alisimulia jana namna ambavyo alimshawishi mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England kubaki Old Trafforf alipokutana naye katika kikao chake cha siri kilichofanyika Juni mwaka jana. Naye Rooney ametoa shukrani zake kwa kocha wake huyo baada ya kusaini mkataba utakaomalizika Juni mwaka 2019. Mkataba huo unamfanya Rooney awe mchezaji anayelipwa zaidi duniani.
Pauni 300,000 kwa wiki
Pauni 43,000 kwa siku
Pauni 1,800 kwa saa
Pauni 30 kwa dakika
50p kwa sekunde
No comments: