» » » Haya ndiyo mambo matatu anayojivunia Mr Blue

Harry Sameer aka Mr Blue wiki hii alizungumza na matandao wa Bongo5 alielezea mambo matatu anayojivunia mpaka sasa kuwa nayo

Mr Blue

Na haya ndiyo mambo matatu anayojivunia Mr Blue

1. Kuwa Hai

Mr Blue anaamini kuwa na uhai na afya njema ndio chanzo cha mambo yote. “Namshukuru Mungu kwakuwa bado napumua na nina afya,” amesema.

2. Kuwa na Mtoto

Rapper huyo ambaye jina lake jingine kwenye muziki ni Kabayser amesema mwaka huu imekuwa mara ya kwanza kusherehekea siku yake ya kuzaliwa akiwa baba wa mtoto wa kiume aitwaye Sameer. “Nimesherehekea birthday nikiwa na mtoto na hii ndio mara ya kwanza,” amesema rapper huyo.

3. Kuishi kwenye nyumba yake mwenyewe

Mwaka huu Mr Blue alihamia kwenye nyumba yake mwenyewe na hicho ni kitu anachojivunia zaidi kuwa nacho kwa sasa.
“Nahisi hata kamwili kanaanza kuja vizuri kwakuwa tunamshukuru Mungu utumwa fulani wa kodi umeondoka, maisha yanaendelea mbele.”

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply