Frans Hoek na Marcel Bout wajajiunga na Van Gaal kama makocha wasaidizi na mholanzi huyo anakuwa kocha wa kwanza kutoka nje kuiongoza Man United. Van Gaal ataanza kazi rasmi baada ya kumalizika kwa fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil ambako anaiongoza Uholanzi akiwa kocha mkuu.
“Siku zote nilikuwa natamani kufanya kazi ligi kuu ya England. Kuwa kocha Manchester United, klabu kubwa duniani, inanifanya nijivune,” alisema Van Gaal. “Niliwahi kucheza mechi Od Traffford kabla na najua namna uwanja huu ulivyo na hamasa. Mashabiki wanapenda mno mpira. Klabu ina maono ya mbali; nami pia nina maono makubwa,Kwa pamoja nadhani tutaweka historia,” aliongeza.
Pia kocha msaidizi Ryan Giggs alisema amefurahi kupata fursa ya kuwa kocha msaidizi huku akidai kuwa Van Gaal ni kocha bora duniani na anajua atajifunza vitu vingi kutoka kwake na kuchangia kadri niwezavyo
No comments: