» » Wanawake Ukosea hapa tu, kwa wanaume

Kuna makosa ambayo wanawake wengi huwa wanafanya,nadhani labda huwa wanawake huwa wanadhani kuwa manual ya jinsi ya ku mu-handle a guy hivi,ila ukweli ni kwamba hakuna kitu kama hicho,na kama wanawake wengi wangekuwa wanajua haya kabla hata ya kuingia katika mahusiano,basi wasingekuwa wanateseka na kuumizwa mara kwa mara.

Kosa #1:Naweza kumbadilisha.
Ingawa kuna msemo wa kuwa “People don’t change,”hakuna mtu anayetilia maanani ,hadi pale anapokutana na mtu ambaye anabidi abadilike,mara nyingi watu wanadai kuwa ,anahitaji tu mtu wa kumuelewa,etc ila ukweli ni kwamba haitakuja kutokea,siyo kwamba hawawezi kubadilika ,wanaweza,ila huwezi kumbadilisha hadi yeye aamue mwenyewe kubadilika.Kama bado hujamuoa na hauko teyari kumvumilia tabia Fulani ,ushauri wa bure,ni bora kuondoka mapema tu.

Kosa#2:Ananichukulia tofauti na wengine.
Nimeona wanawake wengi wazuri  na akili zao unakuta wana-date na mwanaume aliowahi kuwa na michepuko,utajiuliza kuwa nini?,hii ni kwa sababu wanadhani wao ni special,itakuwa tofauti kwao,wengine utasikia,aliachana na mke wake ili kuwa na mimi kwa sababu ananipenda,siyo kwamba wewe ni special case ,labda inaweza kuwa kweli,lakini ukweli ni kwamba YOU ARE NOT,usijaribu kujitoa muhanga nakufikiria kitu kama hicho,sababu mara chache sana hutokea kweli,ila siyo kila siku ijumaa.

Kosa#3:Humsikilizi kwa makini
Wanawake wengi huwa katika kusikiliza wanaume,huwa wanachagua baadhi tu ya maneno wayapendayo wao,mwanaume huweza sema”napenda kweli siku kuja kuoa,ila nimeshindwa kupata mtu atakayenifaa”,wanawake husikia:”nahamu siku nije kuoa”ila hawasikia sehemu iliyobakia ya maneno,kuna mdada mmoja siku alishawahi kuambiwa kuwa,”napenda sana kuja kuoa,ila huwa nachoka mtu baada tu ya miezi miwili ya mwanzo”kilichotokea baada ya miezi miwili akaachika.

Kosa#4:Kumpa point kwa kuwa Honest
Kama mwanaume anaweza kukwambia matatizo yake yote katika mahusiano,matatizo yake kifedha navitu vingine ambavyo vibaya kuhusu yeye,wanawake wengi hudhani kuwa:”ooh,he is honest with me,ana-plan ya mbali na mimi,hataki kuniumiza ndio maana ananiambia yote haya”,wanawake wengi hudhani kuwa wanaume hawawezi kujitangaza tabia zao,ila baadhi ya wanaume huwa wanatoa onyo kabla,wanakujaribu  kama utawakubali na tabia zao.

Kosa#5:Tukifunga ndoa/Tukipata watoto watambadilisha.
Hii haitokei kwa wanaume wote,ila ni moja ya kosa kubwa lakudhani kuwa inaweza kutokea kuwa kweli anaweza kubadilika badae,wanaume wengi wenye tabia ya ku-cheat,wanaweza kuwa na uwezekani mkubwa wakurudia enzi zao,haswa pale mwanamke anapokuwa mjamzito,kwa hiyo kama unadhani kuwa na watoto au kufunga ndoa kutambadilisha,hii itakuwa umeingia chaka.

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply