Aliyekuwa mshindi wa Bongo Star Search, Emmanuel Msuya, ametokea kumpa madam Ritha zawadi ya aina yake ambayo hatoweza sahau maishani mwake, Mshiriki huyo, amepata mtoto wa kike hivi sasa na amepewa jina la Ritha, Kama zawadi fulani hivi aliyopewa madam kwa kumwezesha kumpa mafanikio makubwa Emanuel Msuya naye akaamua kumpa mtoto wake wa kike Jina hilo. Naye madam Ritha kupitia ukurasa wake wa facebook alifunguka baada ya kupata taarifa hizo,
“Naomba kuchukua nafasi hii kutoa pongezi zangu kwa Emmanuel Msuya (Mshindi wa BSS, 2013) kwa kupata mtoto wa kike amempa jina la Rita.Hongera sana!”- alimalizia madam Ritha. Emanuel Msuya ametokea kufanya mambo mengi kutokana na ushindi huo wa BSS ikiwemo pamoja na kufungua studio yake mwenyewe na kujenga nyumba ya kisasa anamoishi hadi hivi sasa.
No comments: