Rapper na Hit Maker wa 'Nakula Ujana' Nay wa Mitego anatarajia kuachia wimbo wake mpya uitwao ‘Nimewaka’ ambapo pia ametoa sababu ya kuachia nyimbo mfululizo.
Nay ambaye aliachia wimbo wa Mr Nay hivi karibuni ameiambia Bongo5 kuwa inambidi aachie wimbo mpya ili kuwapa mashabiki muziki ambao adai wanaupenda.
“Kiukweli kabisa mimi nina mashabiki wengi na wa aina nyingi, kuna mashabiki ambao wanapenda nikiwa nafanya Hip Hop pia nina mashabiki ambao wanapenda mimi nikiimba na bahati nzuri ninashukuru nimeanza ku-maintain sehemu zote mbili. Nikienda kwenye kuimba nafanya vizuri zaidi, nikija kwenye kurap nafanya vizuri zaidi pia na nimeshatoa ngoma ya Mr Nay nayo inafanya vizuri kupita maelezo, kitu ambacho sikuwa na uhakika kama utafanya vizuri kwa sababu huwezi kujua muziki watu wanaupokea vipi. Lakini namshukuru mwenyezi Mungu nashukuru mashabiki wangu, media pamoja na wadau wote,” amesema Nay.
“Pia huu ni wakati kwa watu wangu wa mchaka mchaka narudi tena kwenye ngoma za biashara ninaweza kusema. Inaitwa ‘Nimewaka’ nimewaka nikashasema nimewaka wale watu wangu wanajua namaanisha nini. Huu ni muda wa kuondoa stress na kutuliza moyo na kutumia ulichonacho iwe ni bar iwe mtaani iwe ni wapi. Video ya Mr Nay inatoka panapo majaliwa soon as possible Jumatatu au Jumatano video itakuwa tayari. Nafikiri nikipata nafasi ndani ya weekend ijayo nitakimbia kwenda kushoot video ya wimbo ‘Nimewaka’. Nafikiri ni wimbo ambao utaachana muda mchache sana kati ya audio na video. Ikitoka audio leo nafikiri video inaweza ikatoka wiki inayofuata. Video ya Nimewaka ninaweza nikachukua watu toka Kenya na tukafanyia hapa ndani ama nikaenda Dubai au USA bado nipo kwenye maandalizi ya mwisho.”

No comments: